The chat will start when you send the first message.
1Upole na uamuzi wa kweli nitauimbia, nitakutungia wimbo, wewe Bwana.
2Nitajitafutia ujuzi wa kuifuata njia iliyo yenye kweli yote. Itakuwa lini, ukija kwangu? Nitaendelea kuutakasa moyo wangu humu nyumbani mwangu.
3Sitayaelekeza macho yangu kwenye mambo yasiyofaa, nachukizwa na kufanya mapotevu, hayagandamani na mimi.[#Fano. 20:8,28.]
4Moyo ulio wenye upotovu sharti uondoke kwangu, sitaki kulijua lililo baya.
5Amsingiziaye mwenziwe kinjamanjama ndiye, nitakayemmaliza, mwenye macho makuu na mwenye moyo wa kujivuna simvumilii.
6Macho yangu huwatazama walio welekevu katika nchi, wakae kwangu, naye aifuataye njia yenye kweli yote ndiye atakayenitumikia.[#Fano. 22:11.]
7Afanyae udanganyifu hakai nyumbani mwangu, wala asemaye uwongo hatasimama machoni pangu.
8Kila kunapokucha nitawamaliza katika nchi wote wasiomcha Mungu, nao wote wafanyao maovu nitawang'oa mjini mwake Bwana.[#Fano. 20:26.]