The chat will start when you send the first message.
1Mtukuze Bwana, roho yangu! Navyo vyote vilivyomo ndani yangu mimi na vilitukuze Jina lake lililo takatifu!
2Mtukuze Bwana, roho yangu! Usiyasahau mema yote, aliyokutendea!
3Alikuondolea manza zote, ulizozikora, nayo magonjwa yako yote akayaponya.[#Sh. 32:1.]
4Akazikomboa roho zako kuzimuni, kisha akakufunga kilemba, ndio magawio ya upole.[#Sh. 5:12.]
5Amekushibisha mema, yawe urembo wako; ujana wako ukarudi kuwa mpya kama ule wa kozi.[#Yes. 40:31.]
6Bwana hufanya yenye wongofu na kuwaamulia wote wakorofikao.
7Alimjulisha Mose njia zake, wana wa Isiraeli aliwajulisha matendo yake.[#2 Mose 33:13.]
8Bwana ni mwenye huruma na mwenye utu, tena ni mwenye uvumilivu na mwenye upole mwingi.[#Sh. 86:15; 2 Mose 34:6.]
9Hatagomba kale na kale, wala hatayashika makali siku zote.[#Yes. 57:16.]
10Hatatufanyizia yapasayo makosa yetu, wala hatatulipisha manza, tulizozikora.
11Kwani kama mbingu zinavyokuwa juu ya nchi, ndivyo, upole wake unavyokua kwao wamwogopao.[#Sh. 36:6; Yes. 55:8-9.]
12Kama maawioni na machweoni kunavyokaliana mbali, ndivyo, alivyoyaweka maovu yetu, yatukalie mbali.
13Kama baba anavyowaonea uchungu walio wanawe, ndivyo, Bwana anavyowaonea uchungu wao wamwogopao.
14Kwani yeye anajua, jinsi alivyotuumba, hukumbuka, ya kuwa sisi tu mavumbi.[#1 Mose 2:7; 3:19; Iy. 10:9.]
15Mtu siku zake hufanana nayo majani, huchanua kama ua la porini;[#Sh. 90:5-6; 1 Petr. 1:24-25.]
16lakini upepo ukipita juu yake, haliko tena, wala watu hawapatambui tena mahali, lilipokuwa.
17Lakini upole wake Bwana huwakalia wamwogopao tangu kale hata kale, nao wongofu wake huwakalia wana kwa wana[#Omb. 3:22; Luk. 1:50.]
18kwao walishikao Agano lake na kuliangalia nako kwao wayakumbukao maagizo yake, wayafanye.
19Bwana alikisimamaisha mbinguni kiti chake cha kifalme, ufalme wake unawatawala watu wote pia.
20Mtukuzeni Bwana, ninyi malaika zake! Nanyi wakuu wa vikosi mlio wenye nguvu, mlifanyao Neno lake, mkilisikiliza hilo Neno lake, sauti yake ikitokea![#Sh. 29:1; Yes. 6:1-4; Dan. 7:10.]
21Mtukuzeni Bwana, ninyi vikosi vyake vyote! Nanyi watumishi wake myafanyao yampendezayo!
22Mtukuzeni Bwana, matendo yake yote mahali po pote, anapotawala! Mtukuze Bwana, roho yangu![#Sh. 148.]