The chat will start when you send the first message.
1E Mungu, moyo wangu umetulia na kushupaa, niimbe na kupiga shangwe! Ndio utukufu wangu.[#Sh. 16:9.]
2Amkeni, pango na zeze, niiamshe mionzi ya jua!
3Kwenye makundi ya watu wako nitakushukuru, Bwana nako kwenye wamizimu nitakuimbia.
4Kwani upole wako ni mkubwa, unatutokea toka mbinguni, nako mawinguni unafika welekevu wako.
5Utukuke, Mungu, juu mbinguni! Nazo nchi zote ziuone utukufu wako!
(7-14: Sh. 60:7-14.)6Kusudi wao, uwapendao, wapate kuopoka, mkono wako wa kuume uwaokoe, ukutuitikia!
7Mungu alisema hapo Patakatifu pake: Nikiigawanya nchi ya Sikemu nitapiga vigelegele: ndipo, nitakapolipimanalo bonde la Sukoti.
8Gileadi ni yangu, Manase ni yangu Efuraimu ni kingio la kichwa changu, Yuda ni bakora yangu ya kifalme.
9Moabu ni bakuli langu la kunawia, Edomu ndiko, nitakakovitupia viatu vyangu, nchi ya Wafilisti nitaishangilia.
10Yuko nani atakayenipeleka mjini mwenye maboma? Yuko nani atakayeniongoza mpaka Edomu?
11Si wewe Mungu uliyenitupa, ukakataa kwenda vitani na vikosi vyetu?
12Tujie, utusaidie, tumshinde atusongaye! Kwani watu hawawezi kutuokoa.
13Kwa nguvu yake Mungu na tufanye nasi yenye nguvu! yeye ndiye atakayewakanyaga watusongao.