The chat will start when you send the first message.
1Haleluya! Mwenye shangwe ni mtu amwogopaye Bwana, apendezwaye sana na maagizo yake.[#Sh. 1:1.]
2Wao wa uzao wake watakuwa wenye nguvu sana katika nchi hii, maana wanyokao mioyo vizazi vyao hubarikiwa.[#Fano. 20:7.]
3Malimbiko ya mali yamo nyumbani mwake, nao wongofu wake husimama kale na kale.
4Penye giza mwanga huwazukia wanyokao mioyo, ndio wenye utu na huruma nao wenye wongofu.[#Sh. 37:6.]
5Mtu mwenye huruma kwa kukopesha ataona mema, yeye atayatengeneza mashauri yake, yashinde kwenye hukumu.[#Sh. 41:2.]
6Kwani hatatikisika kale na kale, mwongofu ni mtu atakayekumbukwa kale na kale.
7Masingizio mabaya hayaogopi, moyo wake umeshupaa, maana humwegemea Bwana.
8Kwa kuwa na msingi wa moyo wake haogopi kamwe, mpaka atakapoona, wanavyofanyiziwa wao wamsongao.[#Sh. 91:8.]
9Alizimwaga mali zake, akawagawia wao waliozikosa; huu wongofu wake hukaa kale na kale, baragumu lake huwa limeelekezwa juu kwa kuwa lenye utukufu.[#2 Kor. 9:9.]
10Asiyemcha Mungu anaviona na kukasirika, hukereza meno, mwisho hupotea, tamaa zao wasiomcha Mungu huangamia.[#Sh. 35:16.]