Mashangilio 113

Mashangilio 113

Kumtukuza Mungu.

1Haleluya! Ninyi watumishi wake Bwana, shangilieni! lishangilieni Jina lake Bwana!

2Jina lake Bwana na likuzwe kuanzia sasa hata kale na kale!

3Toka maawioni kwa jua mpaka machweoni kwake Jina lake Bwana na lishangiliwe!

4Bwana anatukuka kuwapita wamizimu wote, utukufu wake unaupita nao wake mbingu.

5Afananaye na Bwana Mungu wetu yuko nani? Naye alijipatia kao huko juu.[#2 Mose 15:11; Yes. 57:15.]

6Anajinyenyekeza, ayatazame yaliyoko mbinguni nayo yaliyoko nchini.[#Luk. 1:48.]

7Humsimamisha akorofikaye na kumwinua uvumbini, naye mkiwa humkweza na kumtoa kwenye taka,[#1 Mose 41:40-41; 1 Sam. 2:8.]

8amkalishe pamoja nao walio wakuu, kweli pamoja nao wakuu wao wlaio ukoo wake.

9Naye mwanamke akosaye watoto humweka nyumbani kuwa mama ya watoto wenye furaha.[#1 Mose 21:2; 1 Sam. 1:20; 2:21; Luk. 1:57-58.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania