The chat will start when you send the first message.
1Nampenda Bwana, kwa kuwa husikia, huisikia sauti yangu, nikimlalamikia.
2Kwa kuwa hunitegea nami sikio lake, kwa hiyo nitamwitia siku zangu zote.
3Matanzi ya kifo yalikuwa yameninasa, masongano ya kuzimu yakanipata, kwa kuona masikitiko nikasongeka.[#Sh. 18:6; 116:8.]
4Nikalililia Jina la Bwana ya kwamba: Wewe Bwana, iopoe roho yangu!
5Bwana ni mwenye utu na mwenye wongofu, kwa kuwa Mungu wetu hutuonea uchungu.
6Walio kama wachanga Bwana huwalinda; nilipokuwa mnyonge, aliniokoa.
7Rudi, roho yangu, kwenye kituo chako! Kwani Bwana ndiye aliyekutendea mema.[#Sh. 42:6.]
8Maana umeiopoa roho yangu katika kufa, ukafuta machozi machoni pangu, ukaishika miguu yangu, isijikwae.
9Kwa kumtazamia Bwana nitaendelea vivyo hivyo katika nchi zao walio hai.[#Sh. 27:13; 56:13.]
10Nilikuwa nimemtegemea, kwa hiyo na niseme! Lakini nimeteseka sana mimi nami.[#2 Kor. 4:13.]
11Hapo, niliposhikwa na woga, nilisema mimi: Watu wote walioko ni wenye uwongo.[#Rom. 3:4.]
12Nitawezaje kumrudishia Bwana mema yote, aliyonitendea?
13Nitakiinua kinyweo chenye wokovu, kisha nitalitambikia Jina lake Bwana.[#1 Kor. 10:16.]
14Nitamlipa Bwana, niliyomwapia, wote walio ukoo wake wavione na macho yao.[#Sh. 22:26.]
15Ni jambo kuu machoni pa Bwana, wamchao wakifa.[#Sh. 72:14.]
16Mimi nakuomba, Bwana, mimi mtumishi wako, mimi mtumishi wako ni mwana wa mjakazi wako, nawe umenifungulia mafungo yangu.
17Nitakutolea wewe vipaji vya tambiko vya kukushukuru, kisha nitalitambikia Jina lake Bwana.
18Nitamlipa Bwana, niliyomwapia, wote walio ukoo wake wavione na macho yao,
19katika nyua zake Nyumba ya Bwana, katikati mjini mwako, wewe Yerusalemu. Haleluya!