Mashangilio 117

Mashangilio 117

Wote na wamtukuze Mungu!

1Mshangilieni Bwana, ninyi wamizimu wote! ninyi makabila yote ya watu, msifuni![#Rom. 15:11.]

2Kwani upole wake hutenda makuu kwetu sisi, nao welekevu wake Bwana ni wa kale na kale! Haleluya![#2 Mose 34:6.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania