Mashangilio 12

Mashangilio 12

Wamchao Mungu hutulia, ijapo wasingiziwe.

1Okoa, Bwana! Kwani wamekwisha wao wakuchao, nao wakutegemeao wametoweka kwenye wana wa watu.

2Kila mtu na mwenzake husemeana yaliyo uwongo, midomo yao husema yenye ujanja, kwa kuwa wenye mioyo miwili.[#Sh. 73:11.]

3Bwana na akomeshe midomo yote yaliyo yenye ujanja, nazo ndimi zisemazo maneno makuu tu!

4Ndio wanaosema: kwa nguvu za ndimi zetu tutashinda sisi, nayo mikono yetu hutusaidia; yuko nani atakayetutawala?[#Sh. 73:8-9.]

5Kwa ajili ya taabu zao walio wanyonge na kwa ajili ya yowe zao walio wakiwa nitainuka sasa, ndivyo, Bwana asemavyo, niwapatie wokovu wauchuchumiao.

6Maneno ya Bwana ndiyo maneno yaliyo mang'avu hufanana na fedha zilizoyeyushwa chunguni huku nchini, zilizong'azwa hivyo mara saba.[#Sh. 19:9.]

7Wewe, Bwana, utayaangalia! Nasi utatuokoa katika uzazi huo kale na kale!

8Wasiokucha huendelea na kutuzunguka, kwani maoneo ndiyo yanayotukuzwa kwao watu.[#Fano. 28:12.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania