The chat will start when you send the first message.
1Nilipomwita Bwana katika masongano yangu, akaniitikia.
2Bwana, iponye roho yangu, nisishindwe nao wanaonijia kwa midomo yenye uwongo na kwa ndimi za kudanganya!
3Ninyi ndimi zenye udanganyifu, atawapa nini? Kisha yako mambo gani tena, atakayoendelea kuwapatia ninyi?
4Maana zinakuwa kama mishale ya mpiga vita iliyotiwa ukali, au kama makaa ya mshuluti yaliyo yenye moto mwingi.
5Ukiwa wangu ni kukaa ugenini huku Meseki na kutua katika mahema yao watu wa Kedari.[#1 Mose 10:2; 25:13.]
6Kwa kukaa huku siku nyingi roho yangu inahangaika, maana watu wa huku huuchukia nao utengemano.
7Mwenye utengemano ndio mimi, lakini ninaposema nao, wao hutafuta magomvi.