The chat will start when you send the first message.
1Ninayainua macho yangu na kuyaelekeza milimani, kwani ndiko, utakakotoka msaada wangu.[#Yes. 30:29.]
2Msaada wangu hutoka kwake Bwana, ndiye aliyeziumba mbingu na nchi.[#Sh. 124:8.]
3Hatautoa mguu wako, uje kujikwaa, maana halali usingizi akulindaye.
4Tazameni! Halali usingizi, wala hasinzii yeye aliye mlinzi wake Isiraeli.
5Bwana ndiye akulindaye, Bwana ni kivuli chako kuumeni kwako,
6mchana jua lisikuumize, wala mwezi usiku.
7Bwana atakukingia mabaya yote, atailinda roho yako.[#4 Mose 6:24.]
8Bwana na akulinde kutoka kwako na kuingia kwako kuanzia sasa hata kale na kale!