Mashangilio 122

Mashangilio 122

Kuuombea Yerusalemu.

1*Niliwafurahia walioniambia: Twende Nyumbani kwa Bwana![#Sh. 26:6-8.]

2Hivyo miguu yetu iko ikisimama malangoni kwako, Yerusalemu.

3Yerusalemu umejengwa tena kama mji ulioungamanishwa vema.

4Ndiko, mashina ya watu yanakopanda, yaliyo mashina ya Bwana; ndiko, wanakowashuhudia Waisiraeli, walishukuru Jina la Bwana.

5Kwani viti vya uamuzi vilipowekwa, ndipo pale, ni viti vya kifalme vya mlango wa Dawidi.

6Uombeeni Yerusalemu utengemano, watengemane nao waupendao![#Zak. 4:7.]

7Sharti uwe utengemano ndani ya boma lako, nao utulivu katika majumba yako yaliyo mazuri mno.

8Kwa ajili yao walio ndugu zangu na rafiki zangu na niseme tena na kuomba: Utengemano na uwe kwako!

9Kwa ajili ya Nyumba ya Bwana Mungu wetu na nikutafutie mema.*

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania