Mashangilio 124

Mashangilio 124

Kumsifu mwokozi wetu.

1Kama Bwana asingalikuwa nasi, Waisiraeli na waseme hivyo:

2Kama Bwana asingalikuwa nasi, watu walipotuinukia,

3wangalitumeza, tukingali wazima bado; ilikuwa hapo, moto wa makali yao ulipotuunguza.

4Maji mengi yangalitudidimiza hapo, mito ilipopita juu yetu,[#Sh. 42:8; 69:16.]

5kwani hapo mafuriko ya maji yaliyopita juu yetu yangalitutosa kweli.

6Bwana na asifiwe! Kwani hakututoa, tunyafuliwe na meno yao!

7Roho zetu zimepona, kama ndege anavyopona tanzini, kamba za tanzi zikikatika; ndivyo, sisi tulivyopona nasi.

8Msaada wetu uko katika Jina la Bwana, ndiye aliyeziumba mbingu na nchi.[#Sh. 121:2.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania