Mashangilio 125

Mashangilio 125

Mungu huwalinda walio wake.

1Wamwegemeao Bwana hufanana nao mlima wa Sioni, hautikisiki, unakaa kale na kale.

2Kama milima inavyouzunguka mji wa Yerusalemu, ndivyo, Bwana anavyowazunguka walio ukoo wake kuanzia sasa hata kale na kale.[#Sh. 36:7.]

3Kwani bakora yao wasiomcha Mungu haitashika uflame wa kulitawala fungu lao walio waongofu, kusudi waongofu wasiipeleke mikono yao kushika yenye mapotovu.

4Bwana, walio wema wafanyizie mema, nao wanyokao mioyo!

5Lakini wao wazigeuzao njia zao kuwa za kuptokapotoka Bwana an awaache, wajiendee pamoja nao wafanyao maovu! Utengemano na uwakalie wao Waisiraeli![#Gal. 6:16.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania