Mashangilio 128

Mashangilio 128

Mbaraka yao wamchao Mungu.

1Mwenye shangwe ni kila amwogopaye Bwana, azishikaye njia zake!

2Kwani utajilisha yayo hayo, mikono yako iliyoyasumbukia, kwa kuyapata hayo mema yako nawe u mwenye shangwe.

3Mke wako wa nyumbani mwako atafanana na mzabibu uzaao vizuri: watoto wako wataizunguka meza yako kama makuti ya mchikichi.[#Sh. 127:3.]

4Kwani ndivyo, mtu anavyobarikiwa akimwogopa Bwana.

5Bwana na akubariki toka Sioni, uyatazame mema ya Yerusalemu! Na uyaone na kuyafurahia siku zako zote za kuwapo,[#Sh. 134:3.]

6na uone nao watoto wa wanao! Utengemano na uwakalie Waisiraeli![#Sh. 125:5; Gal. 6:16.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania