Mashangilio 133

Mashangilio 133

Mbaraka ya mapatano ya ndugu.

1Utazameni wema na utamu ulioko huko, ndugu wanakokaa pamoja na kupatana

2Ni kama yale mafuta mazuri ya kichwani pake Haroni, yakishuka na kuziiingia ndevu zake zilizokuwa ndefu, zikafika mpaka kwenye pindo la kanzu yake.[#2 Mose 29:7; 30:23-30.]

3Au ni kama umande ulioko Hermoni, nako kwenye milima ya Sioni unakufika. Kwani Bwana alikoagizia mbaraka, ndiko huko, kuwa kwenye uzima kale na kale.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania