The chat will start when you send the first message.
1Haleluya! Lishangilieni Jina lake Bwana! Mlio watumishi wake Bwana, shangilieni!
2Nanyi msimamao Nyumbani mwake Bwana, nanyi mlioko nyuani penye Nyumba ya Mungu wetu,
3mshangilieni Bwana! Kwani Bwana ni mwema. Liimbieni Jina lake na kupiga mazeze! Kwani ni zuri.
4Kwani Bwana alimchagua Yakobo, awe wake, yeye Isiraeli awe mali zake.[#2 Mose 19:5-6; 5 Mose 7:6.]
5Kwani mimi ninajua, ya kuwa Bwana ni mkuu, ya kuwa Bwana wetu anaipita miungu yote kwa huo ukuu.[#Sh. 86:8.]
6Yote, apendezwayo nayo, Bwana huyafanya, ikiwa mbinguni au nchini, ikiwa baharini au kilindini pawapo pote.
7Yeye ndiye anayepandisha mawingu akiyatoa mapeoni kwa nchi, yeye ndiye anayefanya umeme na mvua pamoja, yeye ndiye anayeutoa nao upepo malimbikioni kwake.[#Yer. 10:13.]
8Yeye ndiye aliyewapiga kule Misri wazaliwa wa kwanza akianzia kwa watu, akimalizia kwao nyama.[#2 Mose 12:29.]
9Yeye ndiye aliyetuma vielekezo na vioja, vikutokee kwako, wewe Misri, vimshinde Farao na watumishi wake wote.[#Sh. 78:43-52.]
10Yeye ndiye aliyepiga wamizimu wengi, akaua nao wafalme wenye nguvu,
11kama Sihoni, mfalme wa Waamori, na Ogi, mfalme wa Basani, hata nchi zote za Kanaani pamoja na wafalme wao.[#4 Mose 21:21-35.]
12Akazitoa nchi zao, zitwaliwe, zitwaliwe nao walio ukoo wake wa Isiraeli, ziwe fungu lao.[#Yos. 12.]
13Bwana Jina lako ni la kale na kale, Bwana, ukumbuko wako ni wa vizazi na vizazi.[#Sh. 102:13.]
14Kwani Bwana atawaamulia walio ukoo wake kwa kuwaonea uchungu walio watumishi wake.[#5 Mose 32:36,43.]
(15-20: Sh. 115:4-11.)15Vinyago vya wamizimu ni fedha na dhahabu, mikono ya watu ndiyo iliyovifanya:
16vinywa vinavyo, lakini havisemi, macho vinayo, lakini havioni,
17masikio vinayo, lakini havisikii; wala pumzi hazimo vinywani mwao.
18Kama hivyo vilivyo, ndivyo, watakavyokuwa nao waliovifanya; nao wote pia waviegemeao.
19Mlio wa mlango wa Isiraeli, mtukuzeni Bwana! Mlio wa mlango wa Haroni, mtukuzeni Bwana![#Sh. 118:2-4.]
20Mlio wa mlango wa Lawi, mtukuzeni Bwana! Mmwogopao Bwana, mtukuzeni Bwana!
21Bwana na atukuzwe mle Sioni, yeye akaaye Yerusalemu! Haleluya!