The chat will start when you send the first message.
1Kwa moyo wangu wote nitakushukuru, nitakuimbia na kupiga zeze mbele ya miungu.[#Sh. 82:1.]
2Penya Nyumba yako takatifu nitakutambikia, nalo Jina lako nitalishukuru kwa ajili ya upole wako na kwa ajili ya welekevu wako, kwani umelikuza Jina lako kwa kufanya mambo yapitayo yote, uliyoyasema.[#Sh. 26:8.]
3Siku, nilipokuita, uliniitikia, ukaishupaza roho yangu na kuitia nguvu.
4Bwana, wafalme wote wa nchi watakushukuru watakapokuwa wameyasikia maneno, kinywa chako kiliyoyasema.[#Yes. 2:3.]
5Watakapozishika njia za Bwana wataimba, ya kuwa utukufu wa Bwana ni mkubwa.
6Kwani Bwana huko juu aliko humtazama mnyenyekevu, lakini mwenye majivuno anamjua, akiwa yuko mbali bado.[#Sh. 113:5-6.]
7Kama ninaendelea kusongeka po pote, unanishika moyo, nisizimie; makali ya adui zangu uliyainulia mkono wako. mkono wako wa kuume ukaniokoa.
8Bwana atanimalizia jambo hili, upole wako, Bwana, ni wa kale na kale. Kazi za mikomo yako usiziache![#Fil. 1:6.]