Mashangilio 140

Mashangilio 140

Kuomba wokovu kwenye watu wabaya.

1Bwana, kwenye watu wabaya niopoe!

2nilinde, watu wenye makorofi wasinijie!

3Ndio wanaowaza mabaya mioyoni mwao, nao hufanya magomvi kila siku.

4Wamezinoa ndimi zao, ziwe kama za nyoka, sumu ya pili imo midomoni mwao.[#Rom. 3:13.]

5Niangalie, Bwana, mikono yao wasiokucha isinikamate! Nilinde, watu wenye makorofi wasinijie! Ndio wawazao, jinsi watakavyonikumba, nije kujikwaa

6Wenye majivuno wamenitegea matanzi na nyugwe, wakanitandikia nyavu kandokando ya njia, wakaiweka nayo mitego yao, waninase.

7Nikamwambia Bwana: Wewe ndiwe Mungu wangu! Bwana, zisikilize sauti za malalamiko yangu![#Sh. 22:11.]

8Bwana uliye Bwana wangu mwenye nguvu, u wokovu wangu, unakikingia kichwa changu siku za mapigano.

9Bwana, wasiokucha usiwape wanayoyatamani! Wala usiwamalizie mashauri yao mabaya, wasijivune!

10Sumu zao wanizungukao nazo njama zao, walizozisema za kupotoa, na ziwarudie wenyewe na kuwafunika![#Sh. 7:17.]

11Na awanyeshee mvua ya makaa ya moto! Na awakumbe, waanguke, motoni namo mashimoni, wasiweze kabisa kuinuka tena!

12Mtu mwenye masingizio hatashikizwa katika nchi, mtu mwenye makorofi mabaya na yamkimbize, mpaka aangamie!

13Ninajua, ya kuwa Bwana atamwamulia aliye mnyonge, nayo mashauri ya wakiwa atayanyosha.

14Watakaolishukuru Jina lako kweli ndio waongofu, nao wanyokao mioyo watakaa usoni pako.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania