The chat will start when you send the first message.
1Bwana, sikiliza, nikikuomba, uangalie, nikikulalamikia! kwa kuwa u mwelekevu na mwongofu, na uniitikie!
2Usije kwa mtumishi wako, upate kumhukumu! Kwani kwao wote walio hai hakuna aliye mwongofu.[#Sh. 130:3; Iy. 9:2; Rom. 3:20,23.]
3Kwani adui yangu ameikimbiza roho yangu, akaniponda na kuniangusha chini akitaka kuniua, akanikalisha kwenye giza kama wao waliokufa kale.
4Roho yangu ikataka kuzimia kifuani mwangu, moyo wangu humu mwilini ukaguiwa na kituko.
5Nikazikumbuka siku zilizopita kale, nayo matendo yako yote nikayachanganya, mikono yako iliyoyafanya nikayawaza yote.[#Sh. 77:6.]
6Kisha nikakunyoshea mikono yangu, roho yangu ikakutunukia kama nchi kavu.[#Sh. 42:2-3; 63:2.]
7Bwana, niitikie upesi! Roho yangu imemalizika; usinifiche uso wako, nisije kufanana nao washukao kuzimuni![#Sh. 28:1.]
8Unipe kusikia asubuhi mambo ya upole wako! Kwani nimekuegemea. Nijulishe njia, nitakayoishika! Kwani nimekuinulia roho yangu.
9Niopoe, Bwana, ukinitoa kwao walio adui zangu! Nimekukimbilia, unifunike!
10Kwa kuwa Mungu wangu nifunze kufanya yakupendezayo! Roho yako njema iniongoze, nishike njia inyokayo![#Sh. 25:5.]
11Bwana, kwa ajili ya Jina lako nirudishe uzimani! Kwa ajili ya wongofu wako nitoe katika masongano![#Sh. 23:3; 119:25.]
12Kwa ajili ya upole wako wamalize adui zangu! Waangamize wote waisongao roho yangu! Kwani ni mtumishi wako.[#Sh. 116:16.]