Mashangilio 150

Mashangilio 150

Kumshangilia Mungu.

1Haleluya! Mshangilieni bwana hapo Patakatifu pake! Bomani mwake mwenye nguvu mshangilieni!

2Kwa ajili ya matendo yake ya nguvu mshangilieni! Kwa ajili ya ukuu wake mwingi mshangilieni!

3Kwa kuvumisha mabaragumu mshangilieni! Kwa kupiga mapango na mazeze mshangilieni!

4Kwa kupiga patu na kucheza ngoma mshangilieni! Kwa kupiga vinanda na mazomari mshangilieni

5Kwa kupiga matoazi yaliayo vizuri mshangilieni! Kwa kupiga matoazi yenye mavumo sana mshangilieni!

6Na wamshangilie Bwana wote wenye pumzi! Haleluya![#Sh. 41:13; Ufu. 5:13.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania