The chat will start when you send the first message.
1E Bwana, sikia jambo liongokalo! Yaitikie malalamiko yangu! Sikiliza nikuombayo na midomo isiyodanganya!
2Wewe uniamulie shauri langu, maana macho yako huyatazama yaliyonyoka.[#Sh. 43:1.]
3Umeujaribu moyo wangu na kunikagua usiku, ukaning'aza motoni pasipo kuona kibaya; nikajikaza moyoni kwa ajili ya kinywa changu, kisipite mpaka.[#Sh. 16:7; 139:1.]
4Matendo ya mtu yalivyo, ndivyo, midomo yake iumbuavyo; mimi nimejiangalia, nisizifuate njia zao walio wakorofi.
5Miguu yangu hushika sawasawa, uiongozapo, nazo nyayo zangu hazikutangatanga.
6Mimi nikakuita, Mungu, kwani huniitikia; unitegee sikio lako, usikie ninayokuambia!
7Toa magawio yako yastaajabishayo! Kwani huwaokoa wakujeteao, kwa nguvu ya mkono wako huwatoa mikononi mwao wawainukiao.[#Sh. 4:4.]
8Nilinde na kuniangalia kama mboni ya jichoni! Nifiche kivulini mwa mabawa yako![#5 Mose 32:10.]
9Nisiwaonekee waovu wanikorofishao, wala wachukivu wangu waizungukao roho yangu!
10Mioyo yao migumu huishupaza, navyo vinywa vyao husema majivuno.
11Tukiwa tunajiendea tu, mara hutuzuia wakitumbuliza macho, wapate kutuangusha chini.
12Hufanana na simba atamaniye kunyafua, au na mwana wa simba anyatiaye na kujifichaficha.[#Sh. 10:9.]
13Inuka, e Bwana! Umjie mbele, upate kumbwaga! Kwa upanga wako iokoe roho yangu mikononi mwake asiyekucha!
14Mkono wako, Bwana, uniokoe mikononi mwa waume, ambao kiume chao ni cha dunia hii, fungu lao nalo liko nchini tu. Matumbo yao uyajaze mali zako, washibe pamoja na wana wao, tena watakazozisaza waziachie hao watoto wao![#Luk. 16:25; Fil. 3:19.]
15Lakini mimi kwa hivyo, nilivyo mwongofu, nautazamia uso wako, niamkiapo nipate kushiba kwa kukuona, ulivyo wewe.
Akasema