The chat will start when you send the first message.
1Mbingu zinausimulia utukufu wake Mungu, yaliyoko juu huyatangaza matendo ya mikono yake.[#Rom. 1:19-20.]
2Siku huambia siku mwenziwe utume huo, nao usiku huutambulisha usiku mwenziwe.
3Hakuna msemo wala maneno, sauti zao zisisikilike mumo humo.
4Uvumi wao ulitokea katika nchi zote, nayo maneno yao yalifika hata mapeoni kwa ulimwengu; hata jua alilionea kituo hukohuko.[#Rom. 10:18.]
5Nalo hutokea, kama mchumba anavyotoka chumbani mwake, hufurahia kupiga mbio njiani kama mpiga vita.
6Kwenye mwisho wa mbingu ndiko, linakokucha, huendelea, mpaka lichwe kwenye mwisho wake mwingine, hakuna panapojificha, lisipawakie.[#Sh. 104:19.]
7Maonyo yake Bwana yanayo kweli yote, hutuliza roho; ushahidi wake Bwana hutegemeka, hupambanusha wapumbavu.[#Sh. 119:50,130.]
8Maagizo yake Bwana hunyoka, hufurahisha mioyo, amri zake Bwana hung'aa, huangaza macho.[#Sh. 12:7; 18:31; 119:105.]
9Kumwogopa Bwana hutakasa, kutakuwapo kale na kale; maamuzi yake Bwana ni ya kweli, yote pamoja yameongoka.
10Hayo hutunukiwa kuliko dhahabu, hupita hata dhahabu nyingi zilizong'azwa; tena ni matamu kuliko asali, hupita nao ute wa masega yenye asali.[#Sh. 119:72.]
11Kisha mtumwa wako huonywa nayo, kuyashika huleta mapato mengi.
12Yuko nani ajuaye po pote, alipopotelewa? Uning'aze, yaniondokee nayo makosa yajifichayo![#Iy. 9:3; Sh. 130:3.]
13Nako kwao wanaokusahau umtoweshe mtumwa wako, wasinitawale! Ndivyo, nitakavyokuwa pasipo kosa, nipate kutakata, yakiniondokea maovu, yaliyokuwa mengi.[#Sh. 18:24.]
14Maneno ya kinywa changu sharti yakupendeze, nayo mawazo ya moyo wangu sharti yawe wazi mbele yako, Bwana, wewe ndiwe mwamba wangu na mkombozi wangu.