Mashangilio 20

Mashangilio 20

Kumwombea mfalme vitani.

1Bwana na akuitikie siku ya kusongeka, nalo Jina la Mungu wa Yakobo likuwie ngome![#Fano. 18:10.]

2Na atume kwako msaidiaji atokaye Patakatifu pake! Namo Siyoni atokee atakayekushikiza!

3Na avikumbuke vipaji vyako vyote, ulivyovitoa vya tambiko! Nazo ng'ombe zako za tambiko, ulizomchomea, zimpendeze!

4Moyo wako uyatakayo na akupe, nayo mashauri yako yote akutimizie![#Sh. 21:3.]

5Na tushangilie hivyo, anavyokuokoa! Katika Jina la Mungu wetu na tutweke bendera, Bwana atakapokutimilizia yote, uliyomwomba.

6Sasa nimejua, ya kuwa Bwana humwokoa, aliyempaka mafuta; akamwitikia mbinguni palipo Patakatifu pake, akamtolea nguvu za kuumeni kwake ziokoazo.[#2 Mose 15:6.]

7Wengine nguvu zao ni magari, nao wengine farasi, lakini sisi tunajikumbusha Jina la Mungu wetu.[#5 Mose 20:1; Yes. 31:1.]

8Hao wakajikwaa, wakaanguka; lakini sisi tukainuka, tukajisimamisha wima.

9Bwana, tunakuomba, mwokoe mfalme! Nasi siku, tutakapokuita, utuitikie!

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania