Mashangilio 23

Mashangilio 23

Bwana ni mchungaji wangu.

1*Bwana ni mchungaji wangu, hakuna nitakachokikosa.[#1 Mose 48:15; Yoh. 10:12-16.]

2Hunipumzisha mawandani penye majani mazuri, hunipeleka nako kwenye vijito, nipate kutua.[#Ez. 34:14; Ufu. 7:17.]

3Huutuliza moyo wangu kwa kuniongoza, nifuate mapito yaongokayo, Jina lake litukuzwe.[#Yer. 31:25.]

4Hata nitakapopita bondeni kwenye giza la kufa, siogopi kibaya, kwani huko nako wewe uko pamoja nami, fimbo yako na mkongojo wako utanishikiza.[#Sh. 46:3.]

5Wanitandikia meza machoni pao wanisongao, ukanipaka mafuta kichwani pangu, nacho kikombe changu hukijaza, mpaka kimwagikie.[#Sh. 36:9.]

6Kweli wema na upole utanifuata siku zote za kuwapo kwangu, nikae Nyumbani mwa Bwana siku zitakazokuwa zote.*[#Sh. 84:4-5; Rom. 8:31-39.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania