Mashangilio 24

Mashangilio 24

Kuja kwake mfalme mwenye nguvu.

(Taz. 2 Sam. 6.)

1Nchi hii ni yake Bwana navyo vyote vilivyomo, hata ulimwengu pamoja nao wakaao humu.[#Sh. 50:12; 1 Kor. 10:26.]

2Kwani yeye aliushikiza kule baharini, nako kwenye majito akaushupaza.[#1 Mose 1:9-10.]

3Yuko nani atakayepanda mlimani kwa Bwana? Tena yuko nani atakayesimama mahali pake patakatifu?[#Sh. 15.]

4Ni mwenye viganja vitakatavyo naye mwenye moyo ung'aao; ndiye asiyejitia katika mambo ya bure, wala hakuapa uwongo.

5Mema, Bwana aliyompatia, atayatwaa, ndio wongofu upatikanao kwake Mungu aliye na wokovu wake.[#Yes. 48:18.]

6Ukoo wao wamtafutao ndivyo, ulivyo, maana hukunyatia wewe, Mungu wa Yakobo, mpaka wauone uso wako.[#Rom. 2:28-29.]

7Yanyosheni malango, yawe marefu! Navyo vilango vya kale vipanueni, mfalme mwenye utukufu apate kuingia![#Yes. 40:3-4.]

8Huyu mfalme mwenye utukufu ndiye nani? Ni Bwana Mwenye nguvu, aliye mshindaji, kweli, Bwana ni mshindaji, hushinda vitani.

9Yanyosheni malango, yawe marefu! Navyo vilango vya kale vipanueni, mfalme mwenye utukufu apate kuingia!

10Huyu mfalme mwenye utukufu ndiye nani? Bwana Mwenye vikosi, yeye ndiye mfalme, mwenye utukufu.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania