The chat will start when you send the first message.
1Naikweza roho yangu, ikuelekee Bwana.
2Mungu wangu, nimekutegemea, sitapatwa na soni, adui zangu wasipate kushangilia kwa ajili yangu mimi.
3Hawatapatwa na soni kabisa wote wakungojeao, watakaopatwa na soni ndio wakupingao bure.[#Yes. 49:23.]
4Unijulishe njia zako, wewe Bwana, nayo mapito yake unifundishe![#Sh. 27:11.]
5Niendeshe, niyafuate mambo yako ya kweli, ukinifundisha, kwani wewe nidwe Mungu aniokoaye. Wewe ndiwe, nikungojeaye siku zote.
6Kumbuka, Bwana, huruma zako na magawio ya upoke wako! Kwani yaliyo ya kale na kale ndiyo hayo.
7Usiyakumbuke maovu, niliyokukosea nilipokuwa kijana, ila unikumbuke kwa upole wako, Bwana, kwani u mwema.[#Iy. 13:26.]
8Bwana ni mwema na mwongofu; kwa hiyo huonya wakosaji, wakiwa njiani bado.
9Huongoza wanyonge, wakiamuliwa, kweli hufundisha wanyonge njia yake.
10Penya upole na kweli ndipo pote, Bwana anapotangulia, kwao walishikao Agano lake nayo mashuhuda yake.
11Kwa ajili ya Jina lako, Bwana, niondolee manza, kwani hizo, nilizozikora, ni nyingi mno.[#2 Mose 34:6-7.]
12Mtu amwogopaye Bwana yuko nani? Ndiye, atakayemfundisha njia ifaayo, aichague.[#Sh. 32:8.]
13Roho yake yeye itakaa palipo pema, nao walio uzao wake wataitwaa nchi.[#Sh. 37:9.]
14Bwana huwawia mwenzao wa njama wao wamwogopao, nalo Agano lake ndilo, analowajulisha.[#Iy. 29:4; Ef. 1:9.]
15Macho yangu humtazamia Bwana mchana kutwa, kwani yeye ndiye anasuaye miguu yangu, ikiwa tanzini.
16Nigeukie, unihurumie! Kwani mimi niko peke yangu na ukiwa wangu.
17Moyo wangu unaposongeka, uupanulie, kisha unitoe, nilipobanwa!
18Utazame unyonge wangu na usumbufu wangu, uniondolee yote, niliyoyakosa!
19Watazame adui zangu! Kwani ni wengi, wakanichukia kwa ukorofi wao uchukizao.[#Sh. 35:19.]
20Uilinde roho yangu, uniponye! Sitapatwa na soni, kwani nimekukimbilia.[#Sh. 16:1.]
21Ung'avu na unyofu sharti unikinge, kwani kingojeo changu ndiwe wewe.[#Iy. 1:1.]
22Mungu, mkomboe Isiraeli katika masongano yake yote![#Sh. 130:8.]