The chat will start when you send the first message.
1Nitakutukuza Bwana, kwani umeniopoa, hukuwapa adui zangu kunifurahia mimi.[#Sh. 35:19,24.]
2Bwana Mungu wangu, nilipokulilia, ndipo, uliponiponya.
3Bwana, umeipandisha roho yangu, itoke kuzimuni; wengine waliposhuka kaburini, ulinirudisha uzimani.[#Sh. 116:3-4.]
4Ninyi mmchao Mungu, mwimbieni Bwana wenu! Mshukuruni, mwakumbushe watu utakatifu wake!
5Kwani makali yake hukaa punde kidogo tu, kuwapa watu uzima ndiko kunakompendeza. Kama jioni tunakwenda kulala wenye kilio, asubuhi kimegeuka kuwa kicheko.[#Yes. 54:7.]
6Hapo nilipokaa salama nilisema moyoni: Sitatikisika kale na kale.
7Bwana, uliponitazama kwa kupendezwa ulikuwa umeushikiza mlima wangu, upate nguvu; lakini ulipouficha uso wako, nikawa nimestuka!
8Ndipo, nilipokulilia, wewe Bwana, Bwana wangu ndiye kweli, niliyemlalamikia:
9Utapata nini, damu yangu ikimwagwa, nishuke kuzimuni? Mavumbi yatakushukuru nayo, yaitangaze kweli yako?[#Sh. 6:6.]
10Sikia, Bwana, uniwie mpole! Bwana, nitokee kuwa msaidiaji wangu!
11Maombolezo yangu umeyageuza kuwa mashangilio, ukanivika nguo za mchezo ukinivua gunia,[#Yoh. 16:20.]
12roho yangu iliyotukuka hivyo, na ikuchezee, isinyamaze. Bwana Mungu wangu, kale na kale nitakushukuru.[#Sh. 16:9.]