The chat will start when you send the first message.
1Wewe Bwana, nimekukimbilia, sitatwezeka kale na kale. Kwa kuwa mwenye wongofu na uniponye!
2Nitegee sikio lako, unisaidie upesi! Niwie mwamba wenye nguvu na nyumba yenye boma! Ndivyo, utakavyopata kuniokoa.[#Sh. 18:3.]
3Kwani mwamba wangu na boma langu ndiwe wewe, kwa ajili ya Jina lako utaniongoza, unipeleke.[#Sh. 23:3.]
4Unitoe katika tanzi, walilonitegea! Kwani aliye nguvu yangu ndiwe wewe.[#Sh. 25:15.]
5Roho yangu naiweka mikononi mwako; Bwana uliye Mungu wa kweli, umenikomboa.[#Luk. 23:46; Tume. 7:59.]
6Nawachukia waangaliao mizimu iliyo ya uwongo tu, mimi ninayemwegemea, ndiye Bwana.
7Nitashangilia na kuufurahia upole wako, kwa kuwa umeutazama ukiwa wangu, ukayatambua nayo masongano ya roho yangu.
8Hukunitia mikononi mwao walio adui zangu, miguu yangu huipatia papana pa kusimamia.[#Sh. 18:37.]
9Niwie mpole, Bwana! Kwani nimesongeka, macho yangu yamenyauka kwa uchungu, nayo roho vilevile pamoja na mwili.[#Sh. 6:8.]
10Kwani siku zangu zimeishia kwa masikitiko, miaka yangu nayo kwa kupiga kite, nguvu yangu imepondeka kwa manza, nilizozikora, hata mifupa yangu haina kiini.
11Nikawa wa kufyozwa tu kwao wanisongao, hata kwa wenzangu wa kukaa nao ni vivyo hivyo, nao rafiki zangu ninawatia woga, wanionao njiani hunikimbia.[#Sh. 69:11-13.]
12Nimesahauliwa mioyoni mwao kama mfu, nikawa kama chombo kilichovunjika.
13Nikasikia wengi, wakinong'onezana: Pande zote pia anastukwia tu; wakanilia njama wote pamoja, wakawaza, ndivyo waone njia ya kunitoa roho.[#Yer. 20:10; 46:5; Mat. 26:3-4.]
14Lakini mimi ninayemwegemea, ndiye Bwana, Mungu wangu ndiwe wewe! Hii naungama.
15Mikononi mwako ndimo, siku zangu za kuwapo zilimo; niponye na kunitoa mikononi mwao adui zangu wanikimbizao![#Sh. 139:16.]
16Uangaze uso wako, mtumishi wako auone! Kwa upole wako na uniokoe![#Sh. 80:4; 4 Mose 6:25.]
17Bwana, usiniache, nisije kutwezwa, kwani nikakulilia; sharti watwezwe wao wasiokucha, na waje kuzimuni kuyamazia huko!
18Midomo yenye uwongo sharti ifumbwe kuwa kimya, kwani mwongofu wamemtolea meneno ya kumkorofisha, kwa majivuno yao wakambeza.
19Ninayastaajabu mema yako, jinsi yalivyo mengi, umeyalimbikia wao wakuogopao, nao wakukimbiliao huwapa machoni pa watu.
20Mafichoni kwa uso wako unawaficha, watu wakiwatolea ukali; ukawafunika chumbani ndani, ndimi zao zikiwagombeza.[#Sh. 27:5.]
21Bwana na atukuzwe! Kwani amenistaajabisha, akaniweka mjini mwenye nguvu kwa upole wake.[#Sh. 17:7.]
22Nami kwa woga wangu nilikua nimesema: Nimetupwa, niondoke penye macho yako, yasinione tena. Lakini malalamiko yangu umeyasikia kweli hapo, nilipokulilia, unisaidie.[#Sh. 116:11.]
23Mpendeni Bwana, ninyi yote mmchao! Bwana huwalinda wamtegemeao. Lakini wafanyao majivuno huwalipisha, asisaze hata kidogo.
24Jipeni mioyo, mpate nguvu, nyote mnaomngojea yeye Bwana![#Sh. 27:14.]