The chat will start when you send the first message.
1*Mwenye shangwe ndiye aondolewaye mapotovu, naye aliyefunikwa makosa yake.[#Rom. 4:6-9.]
2Mwenye shangwe ni mtu, Bwana asiyemhesabia manza, asiyekuwa na udanganyifu rohoni mwake.[#Luk. 18:13.]
3Kwani nilipoyanyamazia, mifupa yangu ikanyauka kwa hivyo, nilivyopiga kite mchana kutwa.[#Sh. 31:11; 51:10.]
4Kwani mkono wako ulinilemea mchana na usiku, kiini cha mifupa kikakauka kama maji penye kiangazi.
5Ndipo, nilipokuungamia makosa yangu, nazo manza, nilizozikora, sikuzifunika; nikasema: Nitamwungamia Bwana mapotovu yangu; ndipo, wewe uliponiondolea manza, nilizozikora kwa kukosa.[#Fano. 28:13.]
6Kwa hiyo kila akuchaye atakubembeleza, siku zitakapotimia; maji mengi yatakapofurika hayatamfikia.
7Wewe nidwe ficho langu, utanilinda, nisisongeke; utanipa, nikushangilie po pote kwa kuniponya.*
8Nitakufundisha na kukuonyesha njia, utakayoishika; macho yangu yatakuelekeza, nikikupa shauri.[#Sh. 25:12.]
9Msiwe kama farasi au nyumbu wakosao akili! Wasipotiwa hatamu na mafungo hawaji kwako.[#Fano. 26:3.]
10Maumivu yake asiyemcha Mungu ndiyo mengi, lakini amwegemeaye Bwana hugawiwa mengi, yamzunguke.
11Mfurahieni Bwana na kumshangilia, ninyi waongofu! Nyote mnyokao mioyo, pigeni vigelegele![#Sh. 33:1.]