The chat will start when you send the first message.
1Nimekuwa nimemngojea yeye Bwana, naye akaniinamia, akakisikiliza kilio changu.
2Akanitoa katika mwina uangamizao, nako kwenye matope yazamishayo, akaisimamisha miguu yangu juu mwambani, nao mwendo wangu akaushupaza.
3Akanipa kinywani mwangu wimbo mpya, nao ni wa kumshangilia Mungu wetu. Wengi wataviona na kuogopa, kisha nao watamwegemea huyu Bwana.[#Sh. 33:3.]
4Mwenye shangwe ni mtu amtumiaye Bwana kuwa egemeo lake, asiyewageukia wajivunao, wala wao wanaodanganya na kutumikia uwongo!
5Bwana Mungu wangu, uliyoyafanya wewe, ni mengi, ni mataajabu yako na mawazo yako yaliyotutokea; hakuna anayefanana nawe wewe. Ninataka kuyatangaza na kuyasimulia, ijapo yawe mengi, yasihesabike.[#Sh. 139:17-18.]
6Ng'ombe na vyakula vya tambiko hakupendezwa navyo, lakini umenizibua masikio yangu; ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa nzima navyo vipaji vya tambiko vya kulipa makosa hukuvitaka.[#Sh. 51:18; Yes. 50:5; Ebr. 10:5-10.]
7Ndipo, niliposema: tazama, ninakuja! Mambo yangu yamekwisha kuandikwa katika kitabu cha kuzingwa.[#Sh. 50:8-13.]
8Kuyafanya, uyatakayo wewe, Mungu wangu, kunanipendeza, nayo Maonyo yako yamo ndani moyoni mwangu,
9nikatangaza yaongokayo, wengi walipokusanyika; itazame midomo yangu, sikuifunga, wewe ulio Bwana unavijua.[#Sh. 22:23,26.]
10Wongofu wako sikuufunika ndani moyoni mwangu, ila welekevu wako na wokovu wako nikausimulia, wala sikuuficha wema wako na ukweli wako, wengi walipokusanyika.
11Huruma zako, wewe Bwana, usininyime, wema wako na ukweli wako unilinde siku zote!
12Kwani makosa yasiyohesabika yalinizunguka, manza, nilizozikora, zikanirudia, nisiweze kuziona zote, ni nyingi sana kuliko nywele za kichwani pangu; ndipo, moyo wangu ulipojiendea, ukanipotelea.
(14-18: Sh. 70.)13Na vikupendeze, Bwana, kuniopoa! Bwana, piga mbio, unisaidie!
14Sharti wapatwe na soni kwa kutwezwa wao wote pamoja walioitafuta roho yangu, waiangamize! Sharti warudishwe nyuma, nyuso ziwaive kwa soni waliopendezwa na mabaya yaliyonipata mimi.[#Sh. 6:10.]
15Sharti waustukie ukiwa wao na kuona soni wale walioniambia: Weye! Weye![#Sh. 35:21,25.]
16Sharti wachangamke na kufurahiwa wote wakutafutao! Waupendao wokovu wako waseme pasipo kukoma: Mkuu ni Bwana!
17Ijapo, niwe mnyonge na mkiwa, Bwana hunikumbuka; msaada wangu na mwokozi wangu ndiwe wewe, Bwana; Mungu wangu, usinikawilie![#Sh. 109:22.]