The chat will start when you send the first message.
1Mwenye shangwe ni mtu atunzaye mnyonge. Naye atakapopatwa na kibaya, Bwana atamwokoa.[#Fano. 19:17; Mat. 5:7.]
2Bwana atamlinda, atampa uzima, aone mema nchini; hutamtoa, adui zake wampate kwa kumtamani.
3Akilala kitandani kwa kuugua, Bwana atamshikiza, amwuguze na kumtandikia vema katika ugonjwa wake wote.
4Mimi nasema: Bwana, nihurumie! Iponye roho yangu! Kwani nimekukosea.[#Sh. 6:3.]
5Adui zangu wananisema vibaya kwa kwamba: Itakuwa lini, atakapokufa, jina lake liangamie?
6Kama mtu anakuja kunikagua, hujisemea ovyo tu, lakini moyo wake huokota ayaonayo kuwa mapotovu, kisha anatoka nje, ayasema.
7Wote wanichukiao hunong'onezana pamoja, watakayonifanyizia, ni mabaya tu, wanayoniwazia kwa kwamba:
8Jambo lisilopona limemkaza, hivyo, anavyolala, hatainuka tena.
9Hata mwenzangu wa uchale, niliyemwegemea kwa moyo, naye anayeula mkate wangu, hunipiga mateke.[#Sh. 55:14; Yoh. 13:18; Tume. 1:16.]
10Lakini wewe Bwana, nihurumie na kuniinua, nipate kuwalipiza!
11Hapo ndipo, nitakapotambua, ya kuwa umependezwa nami, adui yangu asipoweza tena kunipigia yowe.
12Kwa hivyo, mimi ninavyokucha kwa moyo wote, unanishikiza, ukanipa kusimama usoni pako kale na kale.
13Bwana Mungu wa Isiraeli, na atukuzwe kama huko kale, vivyo nazo siku zitakazokuwa kale na kale! Amin. Amin.[#Sh. 72:18; 89:53; 106:48; 150:6.]