The chat will start when you send the first message.
1Moyo wangu umefurika, utunge maneno mema; kwa kumfanyizia mfalme kazi mimi ninayesema. Ulimi wangu ni kalamu ya fundi ajuaye kuandika.[#Sh. 69:1.]
2Wewe unawashinda wana wa watu kwa uzuri wako. Utu umeenezwa midomoni mwako, kwa hiyo Mungu atakubariki kale na kale.[#Imbo. 5:10-16.]
3Funga upanga wako kiunoni, wewe mshindaji! Maana ndio pambo lako na urembo wako.
4Hilo pambo lako na likupe kumaliza kazi! Gombea tu mambo ya kweli na ya upole nayo ya wongofu! Ndivyo, kuume kwako kutakavyokufundisha matendo yatishayo.[#Sh. 72:4.]
5Mishale yako nayo ni mikali; kwa hiyo makabila ya watu yatakuangukia chini, kwani huichoma mioyo yao adui za mfalme.
6Mungu, kiti chako cha kifalme kiko kale na kale pasipo mwisho, nayo fimbo ya ufalme wako ndiyo fimbo inyoshayo mambo ya watu.[#2 Sam. 7:13; Yes. 9:6-7; Ebr. 1:8-9.]
7Ulipenda wongofu, ukachukia upotovu. Kwa hiyo Mungu aliye Mungu wako alikupaka mafuta, haya mafuta ni ya kufurahisha kuliko yale ya wenzio.
8Mavazi yako yote hunukia manemane na udi, hata marashi, kwenye majumba yaliyopambwa na pembe mazeze yanakufurahisha.[#Amo. 3:15.]
9Humo mna watoto wa kike wa kifalme, uliowapamba vizuri, naye mkeo wa kifalme yuko kuumeni kwako, huwa mwenye mapambo ya dhahabu ya Ofiri.
10Sikia mwanangu, uviangalie! Niinamishie sikio lako! Sharti uusahau ukoo wako na nyumba ya baba yako![#1 Mose 2:24.]
11Itakapokuwa, mfalme akutake kwa uzuri wako, basi, kwa kuwa yeye ni bwana wako, sharti umwangukie!
12Wanawake wa Tiro watakutokea usoni, wakupe matunzo, nao wenye mali wa ukoo huu watajipendekeza kwako.
13Mwana wa kike wa mfalme yumo nyumbani mlimo na utukufu, nyuzi za dhahabu tu ndizo zilizoyafuma mavazi yake;
14akivaa nguo za rangi nzuri anapelekwa kwa mfalme, nao watoto wa kike wenzake wamfuatao nyuma wanapelekwa kwako.
15Katikati ya wapiga shangwe na vigelegele watasindikizwa, waje jumbani mwa mfalme kuwa humo.
16Hapo, baba zako walipokuwa, watakuwapo wana wako wa kiume, utawaweka kuwa wakuu katika nchi zote.
17Nitalikumbusha Jina lako kwa vizazi vyote vitakavyokuwa, kwa sababu hii makabila yote ya watu watakushukuru kale na kale,