The chat will start when you send the first message.
1Makabila yote ya watu, yasikilizeni! Nyote mkaao ulimwenguni, yategeeni masikio,
2nyote mlio watuwatu tu, nanyi mlio mabwana! Ninyi mlio wenye mali nanyi maskini, yote pamoja!
3Kinywa changu kitasema yenye werevu wa kweli, nayo mawazo ya moyo wangu ni ya utambuzi.
4Nitaliinamisha sikio langu, lisikie mfano, nitalifumbua fumbo langu na kupiga zeze.[#Sh. 78:2.]
5Siku zikiwa mbaya, niogopeje, watakao kunikorofisha kinyumanyuma wakinizinga?
6Wao wanauegemea uwezo wao na kujivunia mali zao zilizo nyingi.
7Hakuna awezaye kumkomboa ndugu yake, hawezi kumpa Mungu mali za ukombozi.
8Kwani mali za kukomboa roho ya mtu hazilipiki, zinashindakale na kale, hazipatikani.[#Mat. 16:26; 20:28.]
9Ijapo mtu akae sanasana, asilione kaburi,
10lakini hana budi kuliona, maana walio werevu wa kweli hufa, wajinga nao wasiojua kitu huangamia pamoja nao, nazo mali, walizozipata, huziachia wengine.[#Mbiu. 2:16; 6:2.]
11Makaburi yao ni nyumba zao za kukaa kale na kale, ndivyo makao yao ya vizazi na vizazi, hata ikiwa wameita nchi nzima kwa majina yao.
12Hivyo mtu hakai na utukufu wake, hufananishwa na nyama wanaoishilizwa.[#Mbiu. 3:19; 2 Petr. 2:12.]
13Ndiko, zinakokomea njia zao waliojiegemea wenyewe, tena wanafuatwa nao waliopendezwa na maneno yao.
14Kama kondoo wanashurutizwa kwenda kuzimuni, mwenye kuwachunga ndiye kifo. Wanyokao mioyo watawatawala hapo patakapokucha; ndipo, ubishi wao utakapoishia, watakapokaa kuzimuni.
15Kweli Mungu ataikomboa roho yangu katika nguvu ya kuzimuni, naye atakayenipokea ndiye yeye.[#Hos. 13:14.]
16Mtu akipata mali nyingi, usihangaike, ijapo, utukufu wa nyumba yake aukuze kuwa mwingi![#Iy. 21:7-15.]
17Kwani katika hayo yote hayamo, atakayochukua atakapokufa, utukufu wake hautamfuata kwenda kuzimuni![#Mbiu. 5:14-15; 1 Tim. 6:7.]
18Akingali yupo mzima hujituliza mwenyewe, wewe nawe watu watakusifu, ukivila vyako vyenye urembo.[#Luk. 12:19; 16:19-31.]
19Hivyo watu huenda kwenye kizazi cha baba zao, kusiko na mwanga kale na kale wa kuwamulikia.
20Mtu akiwa na utukufu wake, asiutambue, atafananishwa na nyama wanaoishilizwa.[#Sh. 49:13.]