The chat will start when you send the first message.
1Bwana Mungu aliye Mungu kweli alisema, akaziita nchi, akianzia maawioni kwa jua, afike nako machweoni kwake.[#1 Mambo 25:1.]
2Sioni ndimo, utokeamo uzuri usiopitika, maana ndimo, Mungu atokezamo mwangaza wake.
3Mungu wetu anakuja, hanyamazi; moto ulao unamtangulia, upepo uvumao na nguvu unamzinga.[#Sh. 96:13.]
4Anaziita mbingu huko juu, hata nchi za chini, zione, jinsi atakavyowaamulia walio ukoo wake:[#Yes. 1:2.]
5Wakusanyeni kwangu wao wanichao, ndio waliofanya agano na mimi na kunitambikia![#2 Mose 24:4-8.]
6Ndipo, mbingu zilipoutangaza wongofu wake, kwani Mungu aliye mwamuzi ndiye yeye.
7Sikilizeni ninyi mlio ukoo wangu, niseme nanyi, ninyi Waisiraeli, niwashuhudie kwamba: Mungu aliye Mungu wako ndio mimi.
8Kwa ajili ya ng'ombe zako za tambiko sikuonyi, ng'ombe za tambiko, ulizoziteketeza, ziko machoni pangu siku zote.[#Yes. 1:11.]
9Sitachukua madume ya ng'ombe nyumbani mwako, wala mabeberu mazizini mwako.
10Kwani nyama wote wa porini ni wangu, nao wakaao milimani, ni maelfu na maelfu.
11Ninawajua ndege wote walioko vilimani, hata nyama walioko mashambani ni mali zangu.
12Kama ningekuwa na njaa, nisingesema na wewe, kwani nchi zote navyo vyote vilivyomo ni vyangu mimi.
13Nile nyama za ng'ombe? Au ninywe damu za mbuzi?
14*Kumshukuru Mungu kuwe kwako ng'ombe ya tambiko, ukimlipa yule Alioko huko juu uliyomwapia!
15Siku, utakaposongeka, uniite! Ndipo, nitakapokuokoa, kisha unitukuze![#Sh. 81:8; 91:15; Iy. 22:27.]
16Lakini asiyemcha Mungu humwambia: Sababu gani unayasimulia maagizo yangu? Nacho kinywa chako kinayasemaje maneno ya Agano langu?[#Rom. 2:21-23.]
17Nawe unachukizwa unapoonywa, nayo maneno yangu unayatupia nyuma.
18Ukiona mwizi, ni rafiki yako, tena hufanya bia nao walio wazinzi.[#Ef. 5:11.]
19Kinywa chako unakisemesha yaliyo mabaya, ulimi wako hutunga madanganyo.
20Ukikaa na ndugu yako unamsengenya, naye mtoto wa mama yako unamtukana.
21Hivyo ndivyo, ulivyovifanya, nikavinyamazia; ndipo, uliponiwazia kuwa sawa kama wewe. Kwa hiyo ninakuonya nikivitolea machoni pako.[#Sh. 73:11.]
22Nanyi mliomsahau Mungu, yatambueni, nisije kuwararueni, pasiwepo mponya!
23Kunishukuru ndio ng'ombe ya tambiko initukuzayo; hiyo ni njia ya kumwonyesha mtu wokovu wa Mungu.*