Mashangilio 52

Mashangilio 52

Mapatilizo ya waovu.

3Unajivuniaje ubaya, wewe jitu? Upole wake Mungu uko siku zote.[#1 Sam. 22:9-19.]

4Ulimi wako huwaza, jinsi utakavyoangamiza, unafanana na wembe mkali, wewe mfanya madanganyo.

5Unapenda mabaya kuliko mema, kuliko mambo yaongokayo unao uwongo.

6Unapenda maneno yote yapotezayo, kweli u mwenye ulimi wa udanganyifu.

7Kwa hiyo Mungu naye atakuponda, akutoweshe kale na kale, kwenye kituo chako atakupokonya, akung'oe katika nchi yao walio hai.

8Waongofu wakiviona wataogopa, lakini yeye watamcheka na kusema:[#Sh. 91:8.]

9Mtazameni mtu asiyemweka Mungu kuwa ngome yake! Aliziegemea mali zake kwa kuwa nyingi, akajivunia nguvu zake za kuangamiza watu.

10Lakini mimi nafanana na mchekele wenye majani mengi kwa kukaa Nyumbani mwake Mungu, kwani upole wa Mungu ndio, niliouegemea pasipo kukoma kale na kale.[#Sh. 92:13-15.]

11Nitakushukuru kale na kale kwa matendo yako, nitalingojea Jina lako lipendezalo kwao wakuchao.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania