Mashangilio 54

Mashangilio 54

Kuuomba msaada wa Mungu penye masongano.

3Mungu, kwa ajili ya Jina lako niokoe!

Kwa nguvu zako kuu niamulie!

4Mungu, maombo yangu yasikie na kuyasikiliza maneno ya kinywa changu!

5Kwani wasio wa kwetu wameniinukia, wanaitafuta roho yangu wao wakorofi, lakini yeye aliye Mungu hawamtazami.

6Ninajua: Mungu ndiye anayenisaidia, ndiye anayeishikiza roho yangu.

7Uwarudishie ubaya wao waninyatiao! Kwa maana u mkweli uwamalize!

8Kisha nitakutolea ng'ombe za tambiko kwa kupendezwa, nitalishukuru Jina lako kuwa lenye wema.

9Kwani katika masongano yote umeniopoa, macho yangu yakapata kuwafurahia wachukivu wangu.[#Sh. 59:11.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania