The chat will start when you send the first message.
1Kwa kuwa wako watu wanaonifokea, nihurumie Mungu! Siku zote wananigombeza na kunitesa.[#1 Sam. 21:10-15.]
2Hao wanaonisonga wananifokea siku zote, kwani ni wengi wanaonigombeza kwa majivuno tu.
3Siku, ninaposhikwa na woga, ninakuegemea wewe.
4Kwa kuwa naye Mungu na nilitukuze Neno lake, kwa kumwegemea Mungu sitaogopa kamwe; wenye miili ya kimtu wanifanyieje?[#Sh. 27:1; 118:6; Yes. 12:2; 51:12; Mat. 10:28; Ebr. 13:6.]
5Siku zote huyabishia maneno yangu, waniumize, kwa mawazo yao yote hunitafutia mabaya.
6Wao hujikusanya, waniotee na kupanyatia, nyayo zangu zilipo, kwa sababu wanangojea kuipata roho yangu.
7Kwa ajili ya mapotovu yao hawataona wokovu, watu walio hivyo uwachafukie, Mungu, na kuwakumba![#Sh. 55:24.]
8Siku za kutangatanga kwangu umezihesabu wewe, machozi yangu nayo yakusanye kwako katika kichupa! Najua, yamo katika kitabu chako, umeyaandika.
9Hapo, watakaporudi nyuma adui zangu, itakuwa siku ile, nitakapokuitia; maana hili ninalijua, ya kuwa Mungu yuko upande wangu.
10Kwa kuwa naye Mungu na nilitukuze Neno lake, kwa kuwa naye Bwana na nilitukuze Neno lake.
11Kwa kumwegemea Mungu sitaogopa kamwe; walio watuwatu tu wanifanyieje?
12Niliyokuapia, Mungu, nitakulipa, nikushukuru.
13Kwani umeiopoa roho yangu katika kufa; kweli, hata miguu yangu unaiangalia, isijikwae, ipate kuendelea machoni pa Mungu penye mwanga wao wenye uzima.[#Sh. 116:8; Iy. 33:30.]