The chat will start when you send the first message.
1Ni vya kweli hivyo, mnavyohukumu, ninyi wakuu? nayo maamuzi yenu yananyoka, ninyi wana wa watu?[#Sh. 82.]
2Sivyo! Kwani mioyoni mwenu yamo mapotovu; ndiyo mnayoyafanya, nayo makorofi ya mikono yenu mnayaendesha katika nchi.
3Wasiomcha Mungu hukataa kutii tangu kuzaliwa kwao, wasemao uwongo hupotea hivyo, walivyozaliwa.
4Sumu inayofanana na sumu ya nyoka wao wanayo, wafanana na pili asiyesikia kwa kuyaziba masikio,
5ni yule asiyesikiliza sauti ya mganga, ijapo ajue sana kufinga nyoka kwa huo uganga.[#Mbiu. 10:11.]
6Mungu yavunje meno yao vinywani mwao! Nayo magego ya wana wa simba yang'oe, Bwana!
7Sharti wakauke kama maji yanayojiendea tu, mishale yao sharti iwe, kama haina chembe, watakapoielekeza!
8Wawe kama kovya linalokwenda na kuyeyuka, au kama mimba ya mwanamke iharibikayo pasipo kuona jua.
9Hivyo nayo miiba yenu ikiwa haijakomaa penye miti yao, ataipeperusha kwa ukali wa moto, ijapo iwe mibichi!
10Mwongofu atafurahi akiyaona malipizi hayo, ataiogesha miguu yake katika damu yake asiyemcha Mungu.
11Ndipo, watu watakaposema: kumbe mwongofu hupata! Kumbe yuko Mungu ahukumuye katika nchi![#Sh. 7:9.]