Mashangilio 60

Mashangilio 60

Kuomba kwa mtu aliyeshindwa vitani.

1Mungu, umetutupa na kututapanya; kweli ulikuwa umetuchafukia, lakini utugeukie![#2 Sam. 8:3,13; 10:13,18.]

2Umeitetemesha nchi na kuipasua, sasa ziponye nyufa zake, maana imetingishika.

3Walio ukoo wako umewaonea magumu, ukatunywesha mvinyo za kutupepesusha.[#Yes. 51:17,22.]

4Lakini wao wakuogopao umewapa bendera ya kuinuliana, wapate kuyagombea yaliyo ya kweli.[#Sh. 20:6.]

(7-14: Sh. 108:7-14.)

5Kusudi wao uwapendao wapate kuopoka, mkono wako wa kuume uwaokoe, ukituitikia!

6Mungu alisema hapo Patakatifu pake: Nikiigawanya nchi ya Sikemu nitapiga vigelegele; ndipo, nitakapolipima nalo bonde la Sukoti.

7Gileadi ni yangu, Manase ni yangu, Efuraimu ni kingio la kichwa changu, Yuda ni bakora yangu ya kifalme.[#1 Mose 49:10.]

8Moabu ni bakuli langu la kunawia, Edomu ndiko, nitakakovitupia viatu vyangu, nchi ya Wafilisti itanishangilia.

9Yuko nani atakayenipeleka mjini mwenye maboma? Yuko nani atakayeniongoza mpaka Edomu?

10Si wewe Mungu uliyenitupa, ukakataa kwenda vitani na vikosi vyetu?

11Tujie, utusaidie, tumshinde atusongaye! Kwani watu hawawezi kutuokoa.

12Kwa nguvu yake Mungu na tufanye nasi yenye nguvu! Yeye ndiye atakayewakanyaga watusongao.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania