Mashangilio 64

Mashangilio 64

Kumwomba Mungu wokovu mikononi mwa wachukivu wabaya.

1Mungu, isikie sauti yangu, nikikulalamikia!

2Unilinde, nikae na kutengemana, mchukivu akinitisha!

3Unifiche, njama zao wafanyao mabaya zisinijie, wala fujo yao wafanyao mapotovu!

4Ndimi zao wamezinoa, ziwe zenye ukali kama wa upanga, mishale yao, wanayotaka kuipiga, ni maneno machungu.[#Sh. 57:5.]

5Hujificha, wapate kumpiga mishale amchaye Mungu, mara wanampiga, kisha hawaogopi.[#Sh. 11:2.]

6Hushikana mioyo, wazidishe ubaya, maongezi yao ni hayo tu, jinsi watakavyotega matanzi. Yuko nani atakayeyaona? ndivyo, wanavyosema.[#Sh. 94:7.]

7Huwaza makorofi kwa kusema: Tumeijua mizungu yote. Yaliyomo mioyoni mwao kila mmoja hayachunguziki.

8Lakini Mungu atakapowapiga mishale, mara watakuwa wameumia.

9Ndimi zao ndizo zilizowaangusha, wote watakaowaona hivyo watawasimanga.[#Sh. 7:16.]

10Ndipo, watu wote watakapoogopa, wataungama kwamba: Ni kazi ya Mungu! Ndivyo, watakavyoyatambua matendo yake.

11Hapo mwongofu atafurahia kuwa wa Bwana, amkimbilie, nao wote wenye mioyo inyokayo watashangilia.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania