Mashangilio 67

Mashangilio 67

Kumshukuru Mungu.

1Mungu na atuhurumie atubariki! Auangaze uso wake, atumulikie![#4 Mose 6:24-25.]

2Tupe, tuitambue njia yako katika nchi, tuone kwa mataifa yote, jinsi unavyookoa!

3Na yakushukuru, Mungu, makabila ya watu, kweli wao wa makabila yote ya watu na wakushukuru.[#Sh. 117:1.]

4Makabila yote ya yafurahi na kushangilia, kwani unayaamulia makabila ya watu kwa wongofu, makabila yaliyoko katika nchi huyaongoza.

5Na yakushukuru, Mungu, makabila ya watu, kweli wao wa makabila yote ya watu na wakushukuru.

6Nchi ikiyaotesha vema mazao yake, Mungu aliye Mungu wetu hutubariki.[#Sh. 65:10.]

7Mungu hutubariki, wamwogope wote walioko huku nchini hata mapeoni kwake.[#Sh. 33:8.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania