The chat will start when you send the first message.
1Bwana Mungu wangu, nimekukimbilia wewe. Nisaidie, uniokoe mikononi mwao wote wanikimbizao![#1 Sam. 24:10; 26:19; 2 Sam. 16:5-11.]
2Wasiirarue roho yangu kama simba, wakainyafuanyafua, nisipopata mwokozi![#Sh. 10:8-9.]
3Bwana Mungu wangu, kama yako mambo, niliyoyafanya, kikawamo kipotovu mikononi mwangu,[#Iy. 31:7-34.]
4kama nimemkorofisha mwenzangu, tuliyepatana naye, naye aliyenisonga bure nikamwokoa:
5basi, mchukivu na aikimbize roho yangu, aikamate na kunikanyaga hapo chini, anitoe uzimani, nao utukufu wangu aukalishe mavumbini!
6Inuka, Bwana, kwa makali yako! Jikweze, ukinge moto wa makorofi yao wanisongao! Amka, uje kwangu wewe uliyeagiza kuhukumu.
7Mkutano wa makabila ya watu sharti ukuzunguke, kisha hapo, walipo, urudi kuwa juu yao!
8Bwana ndiye atakayewahukumu watu wote; nami niamulie, Bwana, kwa kuwa mwongofu pasipo kosa, nifanyalo.[#Sh. 18:21-27.]
9Ubaya wao wasiomcha Mungu sharti ukomeshwe, lakini mwongofu umshikize, apate kusimama! Mwenye kujaribu mioyo na mafigo ni wewe, Mungu mwongofu.[#Sh. 104:35; Yer. 11:20; 17:10; Ufu. 2:23.]
10Ngao yangu iko kwake Mungu, naye huwaokoa wao wanyokao mioyo.[#Sh. 3:4.]
11Mungu ni mwamuzi mwenye wongofu, ni Mungu atishaye kila siku:[#Sh. 9:5.]
12mtu akikataa kugeuka, ataunoa upanga wake, nao uta wake ataupinda na kuuelekeza.[#5 Mose 32:41; Omb. 2:4; 3:12.]
13Vyombo viuavyo ndivyo, atakavyopachika humo, nayo mishale yake ataiwakisha moto.
14Mwenye kujifunga, atokeze kiovu, mtazameni: huwa kama mwenye mimba ya kuzaa maumivu, lakini anapozaa, ni madanganyo ya kumdanganya yeye!
15Akiwa amechimba shimo na kulitanua, hutumbukia mwenyewe mlemle mwenye mwina, alioutengeneza yeye.[#Fano. 26:27.]
16Maumivu yake ya kuumiza wengine humrudia kichwani pake, nayo makorofi yake humshukia utosini.
17Kwa ajili ya wongofu wake namshukuru Bwana, naliimbia Jina lake Bwana Alioko huko juu.