Mashangilio 72

Mashangilio 72

Kumwombea mfalme mema.

1Mungu, mpe mfalme kuamua, kama unavyoamua! Naye mwana wa mfalme mpe wongofu ulio kama wako!

2Awahukumu walio ukoo wako kwa wongofu, nayo mashauri yao wanyonge wako ayanyoshe!

3Milima iwe yenye matengemano ya kuwagawia watu, navyo vilima vilevile kwa nguvu ya wongofu![#Sh. 85:9-13.]

4Walio wanyonge kwao atawaamulia, nao wana wao maskini atawaokoa, lakini wakorofi atawaponda.[#Sh. 72:12.]

5Jua likingali liko, watakuogopa wao wavizazi na vizazi, mwezi utakavyoviwakia.

6Atashuka kama mvua inyweshayo uchome, au kama manyunyu ya mvua yalegazayo nchi.

7Mwongofu atachipuka siku, atakazokuwapo; mpaka mwezi utakapokuwa hauko tena, utengemano utazidi.

8Atatawala, bahari inakoanzia, mpaka huko, inakoishia, tena kuanzia kwenye jito kubwa mpaka mapeoni kwa nchi.[#Zak. 9:10.]

9Wakaao nyikani watampigia magoti, sharti walambe mavumbi walio adui zake.[#Yes. 49:23.]

10Wafalme wa Tarsisi na wa visiwa watampelekea matunzo, nao wafalme wa Arabia na wa Saba wataleta mahongo.[#Sh. 68:30; 1 Fal. 10:1-2; Yes. 60:9.]

11Wafalme wote pia watamwangukia, nao wamizimu wote watamtumikia.[#Sh. 2:8,10-12.]

12Kwani atamwopoa maskini amliliaye, hata mnyonge akosaye mwenye kumsaidia.[#Sh. 35:10; Iy. 36:15.]

13Atamhurumia akorofikaye naye mkiwa, aziokoe roho zao walio wakiwa.

14Atazikomboa roho zao mwao wanyang'anyi namo mwao wakorofi, maana damu zao ni zenye kiasi kikubwa machoni pake.[#Sh. 9:13.]

15Na akae akiwa mwenye uzima, wamgawie nazo dhahabu za Arabia! Na wamwombee pasipo kukoma, wamtukuze siku zote.[#Sh. 72:10; 84:10; Mat. 2:11.]

16Vilaji vifurike katika nchi mpaka juu milimani! Miti yake ya matunda na ivume kama miti ya Libanoni! Namo mijini watu na wazidi kuwa wengi kama majani uwandani!

17Jina lake na liwepo kale na kale! Siku zote, jua likingali liko, jina lake na lichipuke, watu wa mataifa yote wajibariki na kulitaja pamoja na kulishangilia.[#1 Mose 12:3; 22:18.]

18Na atukuzwe Bwana Mungu, Mungu wa Isiraeli!

Yeye peke yake ndiye afanyaye vioja!

19Jina lake tukufu na litukuzwe kale na kale!

Nchi zote na zijae utukufu wake! Amin. Amin.

20Huu ndio mwisho wa maombo ya Dawidi, mwana wa Isai.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania