The chat will start when you send the first message.
1Kweli Mungu huwaendea Waisiraeli kwa kuwa mwema, ni wao wenye mioyo iliyong'aa
2Lakini mimi ilikuwa imesalia kidogo, miguu yangu ingalijikwaa; hakuna tena iliyosalia, nyayo zangu zingaliteleza.[#Sh. 94:18.]
3Kwani wenye majivuno naliwaonea wivu nilipowaona wasiomcha Mungu, wakikaa na kutengemana.[#Iy. 21:7.]
4Kwa maana hawaoni maumivu ya kuwaua, tena miili yao hunenepa.
5Katika masumbuko ya kimtu hao hawamo, wala mateso ya watu wengine hayawapati.
6Urembo wao ndio majivuno, mavazi yao ya kujifunika ndio ukorofi.
7Macho yao hujitokeza kwa kunona kwao nyuso, mawazo ya mioyo yao hufuliza kujikuza.[#Iy. 15:27.]
8Kwa ukorofi wao mbaya husema na kufyoza, kila wanaposema hujikweza.
9Maneno ya vinywa vyao huyawazia kuwa ya kimbinguni, lakini ndimi zao husema ya kiulimwenguni.
10Kwa sababu hii watu wa kwao hurudi upande wao wakipenda kujinywesha maji yao mengi.
11Husema mioyoni: Mungu anavitambuaje? Uko utambuzi kwake yeye Alioko huko juu?[#Sh. 10:11.]
12Tazama, hivyo ndivyo, wasiomcha Mungu walivyo, ndivyo, wanavyojituliza kale na kale kwa kulimbika mali.
13Ni bure kweli, nikiuangalia moyo wangu, uwe umetakata, nikiinawa mikono yangu kwa maji yaondoayo makosa?
14Nikawa nimeteseka mchana kutwa, nayo mapatilizo yangu yalikuwa yako kila kulipokucha.
15Kama ningaliwaza kwamba; nami niseme kama wao hao, kweli walio kizazi cha watoto wako ningaliwaacha, nikavunja agano.
16Basi, nikayatia moyoni, niyatambua hayo; lakini nilipoyatazama, yakaniwia mazito,
17mpaka nikapaingia Patakatifu pake Mungu; ndipo, nilipoyatambua kwa kutazama, jinsi mwisho wao ulivyo.
18Kweli uliwaweka penye utelezi, ukawaangusha, wapondeke.
19Kumbe mara wameangamia na kutoweka kabisa! Mwisho wao ukawa wa kuustukia.
20Kama ndoto inavyoisha kwa kuamka, ndivyo, unavyozitowesha sura zao ukiwainukia.
21Hapo, nilipoona uchungu moyoni mwangu, nayo mafigo yangu yaliponiumiza na kunichoma,
22ndipo, mimi nilipokuwa jinga, nisijue kitu, nikawa machoni pako kama nyama.
23*Lakini sasa nitaandamana na wewe pasipo kukoma, maana umenishika kuumeni kwangu,[#Rom. 8:35-39.]
24ukaniongoza njia kwa shauri, ulilolipiga wewe, mwisho utanikaribisha huko, utukufu uliko.
25Huko mbinguni yuko mwingine aliye mwenzangu? Sipendezwi tena na ulimwengu huu nikiwa pamoja nawe.
26Ijapo, mwili wangu uzimie pamoja na moyo wangu, wewe Mungu u mwamba wa moyo wangu, tena u fungu langu la kale na kale.[#Sh. 16:5.]
27Hii ni kweli: Wakukaliao mbali hupotea, unawaangamiza wote wanaokuacha kwa kuzifuata tamaa.
28Lakini mimi naona kuwa vema, nikimkalia Mungu karibu. Bwana Mungu ninamtaka kuwa kimbilio langu, niwasimulie watu matendo yako yote.*