The chat will start when you send the first message.
3Unasema: Itakapofika siku, niliyoiweka, mimi nitatoa maamuzi yanyokayo.
4Ijapo, nchi zitetemeke pamoja nao wazikaliao, mimi ndimi ninayezishikiza nguzo zake.
5*Niliwaambia wenye majivuno: Msijivune! Msielekeze mabaragumu juu, ninyi msionicha!
6Mabaragumu yenu msiyaelekeze juu kabisa, wala msinyoshe shingo mtakaposema!
7Kwani maawioni siko, wala machweoni siko, wala nyikani siko, ukuu utokako.
8Kwani Mungu ndiye anayeamua; yeye ndiye anayenyenyekeza, tena ndiye anayekweza.*[#1 Sam. 2:7.]
9Kwani mkononi mwake Bwana kimo kikombe kilichojaa mvinyo zichemkazo kwa viungo vikali, wote pia wasiomcha Mungu katika nchi huwagawia, wanywe, mpaka wafyonze mashimbi nayo.[#Sh. 60:5; Yer. 25:15-16.]
10Lakini mimi nitamtangaza kale na kale, Mungu wake Yakobo nitamwimbia sifa.
11Nayo mabaragumu yao wasiomcha Mungu nitayavunja yote, lakini mabaragumu yao wamchao yataelekezwa juu.