The chat will start when you send the first message.
1Kwa mwimbishaji, wa kuimbia mazeze. Wimbo wa Asafu wa kushukuru. Mungu hujulikana kwao Wayuda, Jina lake ni kubwa kwao Waisiraeli.[#Yoh. 10:14.]
2Kituo chake kiko huko Salemu, nalo Kao lake liko huko Sioni.[#Sh. 132:13.]
3Huko ndiko, alikovunjia mishale ya upindi, hata ngao na panga na mata yo yote ya kupigia vita.[#Sh. 46:10.]
4Kwa utukufu wako wewe unaogopesha, maana huipita ile milima ya wanyang'anyi kwa kuwa mkubwa.
5Wenye mioyo mikali walitekwa nao, wakalala usingizi kwa kuangushwa wale wenye nguvu wote pia, mikono yao ikawalegea.
6Kwa makaripio yako, Mungu wa Yakobo, waliomo garini waliangushwa, wakazimia roho pamoja na farasi.
7Wewe unaogopesha kweli; atakayesimama mbele yako wewe, moto wa makali yako ukitokea, atapatikana wapi?
8Ulipotangaza maamuzi toka mbinguni, nchi ikashikwa na woga, ikanyamaza kimya;[#Sh. 46:11; Hab. 2:20.]
9ndipo, Mungu alipoinuka kuwaamulia watu, apate kuwaokoa wanyonge wote walioko nchini.
10Kwani makali ya watu nayo hukutukuza, mwisho utauzima nao moto wa makali yao utakapojifunga.
11Mkimwapia, mlipeni Bwana Mungu wenu! Wote wakaao na kumzunguka sharti wampelekee matunzo, kwani yeye hutisha, aogopwe sana,[#2 Mose 15:11; 5 Mose 7:21.]
12huzikata roho zao walio wakuu, nao wafalme wa nchi huwaogopesha.