The chat will start when you send the first message.
1Ninyi mlio ukoo wangu, yasikilizeni mafundisho yangu! Yategeni masikio yenu, msikie, kinywa changu kinavyoyasema!
2Nitakifumbua kinywa changu, kiseme mifano na kuwaambia mafumbo yaliyo ya kale.[#Sh. 49:4-5; Mat. 13:35.]
3Tuliyasikia, tukayajua, maana waliotusimuliani baba zetu.[#2 Mose 13:14; 5 Mose 4:9-10.]
4Nasi tusiyafiche wana wao, wao wa vizazi vijavyo tuwasimulie mashangilio ya Bwana nayo matendo yake ya nguvu ya kustaajabisha, aliyoyafanya yeye.
5Alisimika mashuhuda kwao Wayakobo, akaweka maonyo kwao Waisiraeli, akawaagiza baba zetu, wayafundishe, wana wao wayajue,
6kusudi wao wa vizazi vijavyo nyuma wayajue nao, kwamba nao watakapokua wayasimulie watoto wao,
7wapate kumwegemea Mungu na kumjetea, wasizisahau kazi zake Mungu, wayashike maagizo yake,
8wasiwe kizazi, kama hicho cha baba zao: chenye ubishi na ukatavu, chenye mioyo isiyopaelekea hapo pamoja, tena chenye roho zisizomtegemea Mungu.[#5 Mose 32:5-6.]
9Wana wa Efuraimu walikuwa mafundi wa kupiga mishale, lakini siku ya kupiga vita walirudi nyuma.[#Amu. 2:11-13; 12; 2 Sam. 20.]
10Agano la Mungu hawakulishika, wakakataa kuyafuata Maonyo yake.
11Wakayasahau matendo yake, hata vioja vyake, alivyowaonyesha.
12Alifanya vioja machoni pao baba zao katika nchi ya Misri shambani kwa Soani.[#Yes. 19:11.]
13Alipasua bahari, akawapitisha mlemle akiyasimamisha maji yake kuwa kama ukingo.[#2 Mose 14:21-22.]
14Akawaongoza mchana kwa wingu, nao usiku wote kwa mwanga wa moto.[#2 Mose 13:21.]
15Akapasua magenge kule nyikani, akawapa maji mengi ya kunywa, kama viko vilindi.[#2 Mose 17:6; 4 Mose 20:7-11.]
16Kulikokuwa na miamba tu ndiko, alikotokeza vijito, akavifurikisha maji, yatelemke kama ya mito mikubwa.
17Kisha wakafuliza kumkosea tena, wakakataa jangwani kumtii yule Alioko huko juu.
18Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao, wakitaka kwake vilaji viwapendezavyo rohoni mwao.[#2 Mose 16:3; 4 Mose 11:4.]
19Wakamnung'unikia Mungu wakisema: je? Mungu ataweza kututandikia meza huku nyikani?
20Kweli alipopiga mwamba, maji yakatoka, vijito vikaenda; lakini atawezaje kutupa navyo vilaji? nazo nyama atatupatiaje sisi tulio ukoo wake?
21Naye Bwana alipovisikia alichafuka sana, moto ukawashwa wa kuwala wao Wayakobo, makali yakawafokea wao Waisiraeli.[#4 Mose 11:1.]
22Kwani hawakumtegemea yeye Mungu, wala hawakungojea, awaokoe.
23Naye akaagiza mawingu yaliyoko juu, akaifungua milango ya mbinguni,
24akawanyeshea Mana, wapate kula; ndio ngano zambinguni, alizowapa.[#2 Mose 16:4,14-15.]
25Wakala kila mtu huo mkate wa malaika; hivyo aliwapelekea pamba za njiani za kushiba.
26Kisha akatokeza mbinguni upepo wa maawioni kw ajua, akauvuta nao upepo wa kusini kwa nguvu zake.
27Akawanyeshea mvua kama ya mavumbi, ndio nyama wa kula, ni ndege warukao, wengi mno kama mchanga wa ufukoni.
28Akawaangusha kambini kwao po pote, walipokuwa wamepanga.
29Wakala, wakashiba sana, alipowapa, wazikomeshe tamaa zao;[#4 Mose 11.]
30lakini hizo tamaa zao hawakuziacha, hivyo vilaji vyao vilipokuwa vikingalimo vinywani mwao bado.
31Hapo ndipo, makali ya Mungu yalipomkwea kwa ajili yao, waliokuwa wenye nguvu akawaua, nao vijana wa Isiraeli akawalaza uvumbini.[#4 Mose 11:33.]
32Katika mambo hayo yote wakamkosea tena, hata vioja vyake hawakuvitegemea.
33Kwa hiyo alizimaliza siku zao upesi, wakawa kama mvuke, miaka yao ikapita upesi sana, alipowaangamiza kwa mastuko.
34Napo hapo, alipowaua hivyo, ndipo, walipomtafuta, wakarudi na kumtazamia machana kutwa.[#4 Mose 14:23.]
35Wakamkumbuka Mungu kuwa mwamba wao, ya kuwa yeye Alioko huko juu ni mwokozi wao.
36Lakini hata hapo walimdanganya na vinywa vyao, nazo ndimi zao zikamwongopea;
37nayo mioyo yao haikumwelekea, wala Agano lake hawakulitegemea.
38Lakini kwa kuwahurumia akazifunika manza zao, asiwaangamize, akayarudisha makali yake, yaende nyuma kabisa, asiuchochee moto wote wa machafuko yake.
39Akawakumbuka kuwa wenye miili ya kimtu tu, kuwa upepo upitao pasipo kurudi.[#Sh. 103:14-16.]
40Je? Mara ngapi walimchokoza nyikani, wakamsikitisha jangwani?[#4 Mose 14:22.]
41Mara kwa mara walirudi nyuma, wamjaribu Mungu; ndivyo, walivyomsumbua Mtakatifu wa Isiraeli.
42Hawakukumbuka, ya kuwa ni mkono wake uliowakomboa siku ile ulipowatoa mikononi mwake aliyewasonga.
43Naye ndiye aliyevifanya vielekezo vyake katika nchi ya Misri, navyo vioja vyake shambani kwa Soani:[#Sh. 78:12.]
44maji ya mito yao aliyageuza kuwa damu, wasiweze kuyanywa yale maji yao.[#2 Mose 7:19-20.]
45Akatuma kwao mbu, wawale, hata vyura, wawamalize.[#2 Mose 8:6,24.]
46Mashamba yao akawapa funutu, navyo, vyakula, walivyovipanda na kusumbuka, akawapa nzige.[#2 Mose 10:13.]
47Mizabibu yao akaivunja kwa mvua ya mawe, kwa hiyo mvua ya mawe ikafa nayo mikuyu yao.[#2 Mose 9:25.]
48Hata ng'ombe wao akawatoa, wapigwe nayo hiyo mvua ya mawe, nao mbuzi wao akawamaliza kwa umeme.
49Akatuma kwao moto wa makali yake, tena machafuko na machungu na masongano mengine; lilikuwa kundi zima la malaika waliowapelekea mabaya.
50Akayafungua makali yake, yajiendee tu, hakuzitoa roho zao katika kufa, ila aliwaacha, kipindupindu kiwashike, wajifie.[#2 Mose 9:15.]
51Akampiga kila mzaliwa wa kwanza katika nchi ya Misri, wote waliokuwa malimbuko yenye nguvu katika mahema ya Hamu.[#1 Mose 10:6; 2 Mose 12:29.]
52Lakini walio ukoo wake walitoka, akiwachunga kama kondoo, akawaongoza kama kundi la mbuzi huko nyikani,[#Sh. 77:20.]
53akawasafirisha vizuri, wasishikwe na woga, lakini adui zao bahari iliwafunika.[#2 Mose 14:19,22,27.]
54Akawafikisha kwenye mpaka wa Patakatifu pake, penye ule mlima, ambao ulijipatia mkono wake wa kuume.[#2 Mose 15:17.]
55Akawafukuza wamizimu mbele yao, akawaagiza kugawiana nchi zao kwa kuzipigia kura, kila apate fungu lake, ndilo liwe urithi wake, akayakalisha mashina ya Isiraeli katika mahema yao.
56Lakini walimjaribu Mungu alioko huko juu na kumchokoza, hawakuyashika maagano yake, aliyoyashuhudia,
57wakarudi nyuma kwa udanganyifu wao kama baba zao, wakapinduka kama upindi usiotegemeka.[#Hos. 7:16.]
58Kwa kutambika vilimani juu wakamkasirisha, kwa kuvitambikia vinyago vya wakamtia wivu.[#5 Mose 32:21.]
59Moto wa makali ukamkwea Mungu, alipoyasikia, akawatupa Waisiraeli kabisa kabisa.
60Akaliacha Kao lake kule Silo, ni lile hema, ambalo alikaa humo kwenye watu.[#1 Sam. 1:3; 4:11.]
61Wale, aliowatia nguvu, akawatoa, wafungwe, waliokuwa urembo wake akawatia mikononi mwao waliowasonga.
62Walio ukoo wake akawaacha, wauawe na panga, wao waliokuwa fungu lake akawatolea makali yake.
63Moto ukawala vijana wao wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za ndoa.
64Watambikaji wao wakauawa kwa panga, nao wajane wao hawakuwaombolezea.[#1 Sam. 4:17,20.]
65Kisha Bwana aliamka kama mtu aliyelala usingizi, kama mwenye nguvu anayepiga shangwe akiondoka kwenye mvinyo.
66Akawapiga waliowasonga, akawarudisha nyuma, nayo masimango ya kale na kale ndiyo, aliyowapatia.
67Akakitupa kituo cha Yosefu, nao ukoo wa Efuraimu hakuuchagua.[#Sh. 78:9.]
68Akauchagua ukoo wa Yuda na mlima wa Sioni, alioupenda.[#2 Mambo 6:6.]
69Akapajenga Patakatifu pake, paende juu kabisa, pawe kama nchi, aliyoiweka ya kuwapo kale na kale.
70Kisha akamchagua mtumishi wake Dawidi, aje kumtumikia; kwenye mazizi ya kondoo ndiko, alikomchukua.[#1 Sam. 16:11-12.]
71akamtoa kwenye kondoo wanyonyeshao, awachunge walio ukoo wake Yakobo pamoja nao walio fungu lake Isiraeli.[#2 Sam. 7:8.]
72Akawachunga kwa kuwa mwenye moyo uliotakata wote, kwa kuwa mikono yake iliijua kazi hiyo, akawaongoza.