The chat will start when you send the first message.
1Mungu, wamizimu wameuingia mji ulio fungu lako, wakalichafua Jumba lako lililo takatifu, Yerusalemu wakaugeuza kuwa mabomoke tu.
2Mizoga ya watumishi wako wameitoa, iliwe na ndege wa angani, nayo miili yao wlaiokucha wamewapa nyama wa porini.
3Damu zao wakazimwaga kama maji, zizunguke Yerusalemu, tena hakuna aliyewazika hao waliokufa.
4Majirani zetu tunaona soni kwao, maana watuzungukao wanatufyoza na kutusimanga.[#Sh. 44:14.]
5Bwana, mpaka lini utatukasirikia? Itakuwa kale na kale? Wivu wako unachoma kama moto uwakao.[#Sh. 80:5.]
6Makali yako wamwagie wamizimu wasiokujua, nazo nchi zenye wafalme wasiolitambikia Jina lako![#Yer. 10:25.]
7Kwani wamemla Yakobo, wakapabomoa, walipokuwa amekaa.
8Usizikumbuke manza, baba zetu walizozikora, ukitulipisha sisi! Huruma zako na zije kutufikia upesi! Kwani tumelegea sana.
9Mungu uliye mwokozi wetu, tusaidie, kwa ajili ya utukufu wa Jina lako tuopoe, kwa ajili ya Jina lako yafunike makosa yetu!
10mbona wamizimu waseme: Mungu wao yuko wapi? Sharti tuvione na macho yetu, vikitambulikana kwao wamizimu, jinsi unavyozilipiza damu zilizomwagwa za watumishi wako.[#Sh. 42:4; 115:2; Yoe. 2:17.]
11Sharti hivyo, walio kifungoni wanavyopiga kite, vifike mbele yako, kwa nguvu zamkono wako zilizo kuu uwaokoe kufani hao wanao![#Sh. 102:21.]
12Majirani zetu uwarudishie mara saba vifuani mwao vyote, walivyokusimangia wewe, Bwana![#Sh. 137:7.]
13Ndipo, sisi tulio ukoo wako na kindoo, unaowachunga, tukapokutolea shukrani kale na kale, tukisimulia vizazi na vizazi, ya kuwa inapasa kukushangilia.