The chat will start when you send the first message.
1Bwana Mungu wetu, Jina lako hutukuka sana katika nchi zote, maana umeutanda utukufu wako kule mbinguni.
2Vinywani mwao watoto wachanga namo mwao wanyonyao ulijitengenezea tukuzo, upate kuwashinda wao wakupingiao, upate kumnyamazisha hata mchukivu naye ajilipizaye.[#Mat. 21:16.]
3Ninapozitazama mbingu zako, vidole vyako vilizoziumba, hata mwezi nazo nyota, ulizoziweka wewe,[#Sh. 19:2.]
4basi, mtu ndio nini, umkumbuke? mwana wa mtu naye, umkague?[#Sh. 144:3; Ebr. 2:6-9.]
5Ulimpunguza kidogo, asilingane na wewe, Mungu, lakini macheo na mapambo yenye utukufu ndiyo, uliyomvika.[#1 Mose 1:26.]
6Ukampa kuyatawala yote, mikono yako iliyoyafanya, yote pia ukayaweka kuwa chini miguuni pake:[#Mat. 28:18; 1 Kor. 15:27.]
7kondoo na ng'ombe wote pamoja, nao nyama wa porini,
8hata ndege wa anga nao samaki wa baharini, nao nyama wote waliomo vilindini mwa bahari.
9Bwana Mungu wetu, Jina lako hutukuka sana katika nchi zote.