The chat will start when you send the first message.
1Bwana, ulikuwa umependezwa na nchi yako, tena ulikuwa umerudisha mateka yake Yakobo.
2Walio ukoo wako ukawaondolea manza, walizozikora, makosa yao yote ukayafunika.
3Machafuko yako yote ukayatuliza na kuuzima moto wa makali yako.
4Mungu uliye mwokozi wetu, uturudishe! Ukomeshe uchungu, ulio nao kwa ajili yetu!
5Makali yako yatukalie kale na kale? Au utayaeneza hayo makali yako, yafikie vizazi na vizazi?[#Sh. 77:8.]
6Hutatuchangamsha tena, kwa kuturudisha uzimani, walio ukoo wako wakufurahie?
7Bwana, tupe kuuona tena huo upole wako, ukitugawia wokovu wako sisi nasi!
8Mungu Bwana atakayoyasema, ninataka kuyasikia, kwani wao walio ukoo wake nao wanaomcha huwaambia maneno yenye utengemano, wasirudie tena ujinga wao.[#Sh. 72:3.]
9Kweli wokovu wake uko karibu kwao wamwogopao, utukufu upate kukaa katika nchi yetu.
10Upole na welekevu sharti ukutaniane, nao wongofu na utengemano sharti unoneane!
11Ndivyo, welekevu utakavyochipuka katika nchi, wongofu ukiitazama toka juu mbinguni.
12Ndipo, Bwana atakapotupa hayo mema tena, ndipo, nchi yetu nayo itakapotupa mazao yake tena.
13Utakaokwenda mbele yake ndio wongofu, tena ndio utakaofuata hapo, alipopita, upatengeneze kuwa njia.*